Waziri Sangu aongoza maadhimisho ya miaka 19 ya Kanisa la WRC

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu ameongoza maadhimisho ya miaka 19 ya Kanisa la Huduma ya Neno la Upatanisho (WRC), linaloongozwa na Askofu na Nabii Nicolaus Suguye.

Katika maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Waziri Sangu aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, Mbunge wa Kivule, Ojambi Massaburi pamoja na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, ambapo walipokelewa na waumini na viongozi wa kanisa hilo.

Mbali na viongozi hao, pia walihudhuria viongozi mbalimbali wa dini akiwemo Askofu wa Kanisa la Arise & Shine, Boniphace Mwamposa na Askofu wa Kanisa la Ufunuo Tanzania, Paul Bendera.

Maadhimisho hayo yalipambwa na nyimbo za sifa na shukrani, huku waumini wakionesha furaha na kujivunia mafanikio ya kanisa lao tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Sangu alipongeza huduma inayotolewa na kanisa hilo, akisema imekuwa na mchango mkubwa kwa jamii.

“Tunafurahia kazi ya Mungu mnayoifanya kupitia huduma yenu. Heshima hii umepewa Askofu kwa kazi kubwa uliyoifanya,” amesema.

Waziri Sangu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na taasisi za dini katika kuimarisha maendeleo ya jamii na kudumisha amani nchini.

Amesema taasisi za dini zimekuwa na mchango mkubwa katika malezi ya maadili pamoja na utoaji wa huduma kwa jamii.

Aidha, amewasilisha salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa serikali inaendelea kuthamini mchango wa taasisi hizo katika kuleta mshikamano na maendeleo.

Ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, taasisi za dini zimekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii kwa kutoa misaada kwa wahitaji na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Waziri huyo pia ameahidi kuwa serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi hizo ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mpogolo, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewashukuru viongozi wa dini kwa mchango wao mkubwa katika kudumisha amani na utulivu mkoani Dar es Salaam.

“Tuna kila sababu ya kuwashukuru na kumtukuza Mungu. Hata tulipowahitaji walikuja bila kusita. Mafanikio na utulivu tunaouona leo ni matokeo ya mchango mkubwa wa viongozi wa dini, ambao ni muhimu sana katika mkoa huu.” amesema.

spot_img

Latest articles

Taifa gas yatangaza kutokupandisha bei ya gesi ya majumbani

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taifa Gas imetangaza kuwa haitapandisha bei ya gesi ya majumbani...

Suguye ahimiza Watanzania Kudumisha Amani na Umoja Kuelekea Sikukuu ya Pasaka

Na Mwandishi wetu Watanzania wameaswa kudumisha amani na mshikamano kuelekea sikukuu ya pasaka ili...

Bosi wa mafuta atumbuliwa

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti...

Nishati Safi yafungua milango ya fursa kwa watengeneza maudhui

Na Mwandishi Wetu, Mwanza WATENGENEZA maudhui nchini wamehamasishwa kutumia ubunifu wao kujipatia kipato kupitia fursa...

More like this

Taifa gas yatangaza kutokupandisha bei ya gesi ya majumbani

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taifa Gas imetangaza kuwa haitapandisha bei ya gesi ya majumbani...

Suguye ahimiza Watanzania Kudumisha Amani na Umoja Kuelekea Sikukuu ya Pasaka

Na Mwandishi wetu Watanzania wameaswa kudumisha amani na mshikamano kuelekea sikukuu ya pasaka ili...

Bosi wa mafuta atumbuliwa

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti...