TAFF yajipanga kwa Ligi Kuu, Tabora yaanzisha timu

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu (TAFF), Shaban Msangi ameitembelea timu mpya ya soka kwa watu wenye ulemavu ya Unyanyembe mkoani Tabora ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu Soka, itakayoanza Julai, 2026, jijini Dar es Salaam.

Msangi amesema kutembelea timu hiyo ni moja ya juhudi za shirikisho katika kukuza mchezo wa soka kwa watu wenye ulemavu kwa kuhakikisha wanaifikia mikoa mingi  ili kupata idadi kubwa ya timu kuelekea katika ligi hiyo.

Hata hivyo amesema kuna changamoto wanayokutana nayo, kwa mfano katika timu hiyo ya Unyanyembe kuna uhaba wa vifaa vya michezo kama vile jezi, viatu na magongo na kuwaomba wadau kujitokeza kutoa sapoti.

“Kama tunavyojua mchezo huu ni kwa watu wenye ulemavu, ni watu wenye mahitaji  maalum, ni mchezo ambao umebeba zaidi hisia za watu,” ameeleza Msangi.

Kwa upande wake kocha wa timu hiyo ya Unyanyembe, Hamad Simba amesema wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na ligi hiyo, huku akiwahimiza wakazi wa mkoa huo kupeleka vijana kujiunga na timu.

“Tuna nafasi bado vijana waliopo wilayani, popote pale mkoa wa Tabora waje wajiunge na timu nafasi bado ipo. Lakini pia ombi langu nikipata msaada wa vifaa itasaidia zaidi kujenga timu hii,” amesema.

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this