Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini, Mkoani Lindi, Selemani Bungara maarufu Bwege amefariki leo mchana Machi 30,2026 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya binafsi iliyopo Kigamboni Jijini Dar es salaam,
Kaka wa marehemu aitwaye Abbas Bungara amesema Bwege alifikishwa Hospitalini hapo kwa ajili ya kuendelea na matibabu na ndipo umauti ulivyomfika.
“Kwa sasa mipango ya mazishi inaendelea na taarifa zaidi zitatolewa hapo baadaye ila msiba kwa sasa upo kwangu mimi Kaka yake maeneo ya Temeke,” amesema.
Bwege amewahi kuwa Mwanachama wa CUF, ACT Wazalendo, hivi karibuni amekuwa akionekana kuhudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu makahamani.


