Wanawake TRA Wapongezwa kwa Mchango wa Ukusanyaji Mapato

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, amewapongeza wanawake wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mchango wao mkubwa katika kusimamia na kuhamasisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Akizungumza leo Machi 8, 2026 katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Dkt. Mwamba amesema siku hiyo ni fursa muhimu ya kutambua nafasi ya mwanamke katika utumishi wa umma na katika kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.

Amesema pamoja na kusherehekea siku hiyo, wanawake wanapaswa kukumbushana wajibu wao wa kufanya kazi kwa uadilifu, uwajibikaji, weledi na uaminifu, wakizingatia kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inayosema “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana, Msingi Jumuishi Kufikia Dira ya 2050.”.

Kwa mujibu wa Dkt. Mwamba, kauli mbiu hiyo inaonesha wazi mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kusimamia sera na mifumo inayolinda na kukuza haki na usawa kwa wanawake nchini bila kujali sekta wanazofanya kazi.

“Tunapaswa kutambua kuwa tuna uwezo, na uwezo huo ndio umetufikisha hapa tulipo. Mwanamke anapowezeshwa taasisi inakuwa imara zaidi, na taasisi inapokuwa imara taifa nalo linakuwa imara,” amesema.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, amesema wanawake wa taasisi hiyo wameendelea kuonyesha umahiri, ubunifu na uadilifu mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao.Mwenda amesema kwa sasa TRA ina jumla ya watumishi 8,832, ambapo zaidi ya asilimia 35 ni wanawake, huku akiamini idadi hiyo itaendelea kuongezeka kadri taasisi hiyo inavyoendelea kuajiri watumishi wapya.

“Kwa sasa tuna watumishi 8,832 na zaidi ya asilimia 35 ni wanawake. Ninaamini tunakokwenda idadi hiyo itaongezeka zaidi na huenda wakafanana au hata kuwazidi wanaume,” amesema.

Ameongeza kuwa katika ajira zilizofanyika mwaka jana, zaidi ya asilimia 49 ya walioajiriwa walikuwa wanawake, jambo linaloashiria kuwa taasisi hiyo inaelekea kufikia uwiano wa zaidi ya asilimia 50 ya wanawake katika siku zijazo.

Mwenda pia amesema wanawake wameendelea kupewa nafasi katika nafasi za juu za uongozi kutokana na uwezo wao mkubwa wa kiutendaji, weledi na uadilifu.

“Nafasi nyingi za juu za uongozi TRA zinashikiliwa na wanawake, na sababu kubwa ya kuwateua ni umahiri wao, weledi pamoja na uadilifu mkubwa wanaouonyesha katika kazi zao,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa Fedha wa TRA, Dina Edward, amesema mapato ya kodi huchangia kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo elimu bure, huduma za afya na ujenzi wa miundombinu.

“Wanawake wa TRA ni sehemu muhimu ya mafanikio ya taasisi hii katika ukusanyaji wa mapato na kuvunjwa kwa rekodi za makusanyo katika miezi ya hivi karibuni,” amesema Dina.

spot_img

Latest articles

Mchungaji Kimaro: Miradi ya Familia Ndio Suluhisho la Ajira kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu  MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjiri Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama Dk....

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani: TRA Yakabidhi Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Milioni 40

Na Tatu Mohamed KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8,...

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

More like this

Mchungaji Kimaro: Miradi ya Familia Ndio Suluhisho la Ajira kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu  MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjiri Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama Dk....

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani: TRA Yakabidhi Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Milioni 40

Na Tatu Mohamed KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8,...

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...