Rais Samia azindua jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Februari 24, 2026, amezindua jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa lililojengwa katika eneo la Kikombo, jijini Dodoma, huku akilitaka Jeshi la Tanzania kuhakikisha miundombinu hiyo  inatumika kikamilifu kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa.

Ujenzi wa jengo hilo ulianza wakati wa Serikali ya Awamu ya Tano, ambapo jiwe la msingi liliwekwa Novemba 25, 2019, na aliyekuwa Rais wa awamu hiyo, Hayati John Magufuli.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amesema kuwa jengo jipya la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa ni alama ya ukomavu wa taifa na uthibitisho wa uwezo wa Watanzania kupanga, kuamua na kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia rasilimali na wataalamu wa ndani.

Amesema uwekezaji huo unaimarisha uhuru wa maamuzi ya taifa na kulipa heshima katika masuala ya ulinzi barani Afrika, akibainisha kuwa Tanzania sasa ni miongoni mwa nchi zinazotoa kipaumbele cha juu kwa shughuli za ulinzi.

Amesisitiza kuwa makao makuu hayo yanapaswa kuwa kituo cha fikra, uchambuzi wa kitaalamu na uratibu wa kisayansi wa mikakati ya ulinzi inayoendana na mabadiliko ya wakati.

Rais Samia ameeleza kuwa katika mazingira ya sasa ya usalama wa dunia, ulinzi hauhusiani na silaha pekee, bali unategemea pia upatikanaji na uchambuzi wa taarifa, matumizi ya teknolojia za kisasa, mifumo madhubuti ya mawasiliano pamoja na ubobezi wa hali ya juu wa kitaalamu.


Amebainisha kuwa baada ya kulitembelea jengo hilo, ameridhishwa na hatua zilizofikiwa katika kuzingatia matumizi ya teknolojia na mifumo ya kisasa, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza nguvu katika awamu zijazo za ujenzi.

Aidha ameahidi kuhakikisha kuwa awamu zilizobaki za mradi huo zinakamilishwa kwa wakati ili kuendelea kuimarisha uwezo wa taifa katika kulinda mipaka, maslahi na usalama wa nchi

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda, amesema gharama zilizotumika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo na miundombinu iliyopo ni Sh. 212 bilioni  ambapo fedha zote zimetolewa na Serikali.


“Makao Makuu haya ya kudumu ya ulinzi wa taifa ni ya kwanza kabisa kihistoria katika jeshi letu. Kama wote mnavyojua, kabla ya makao makuu haya, jeshi lilikuwa na makao makuu yake Upanga, Dar es Salaam, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964,” amesema Jenerali Mkunda.

spot_img

Latest articles

MIF 2026 kujadili mikakati ya kufikia uchumi wa kati wa juu 2050

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imesema Mkutano wa Jukwaa la Wakurugenzi wa Bodi na Watendaji...

Kombe la Shirikisho hatua 32 Yanga yaangukia Polisi, Simba B19

Na Winfrida Mtoi DROO ya hatua ya 32 wa Kombe la Shirikisho  msimu wa 2025/26,...

Lissu aibwaga Jamhuri, kesi yahamia Mahakama ya Rufani

Na Mwandishi Wetu MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imekubali mapingamizi...

Wizara ya Madini na CRDB wasaini makubaliano kurahisisha mikopo kwa wachimbaji wadogo

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Madini kupitia Tume ya Madini leo Februari 23, 2026...

More like this

MIF 2026 kujadili mikakati ya kufikia uchumi wa kati wa juu 2050

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imesema Mkutano wa Jukwaa la Wakurugenzi wa Bodi na Watendaji...

Kombe la Shirikisho hatua 32 Yanga yaangukia Polisi, Simba B19

Na Winfrida Mtoi DROO ya hatua ya 32 wa Kombe la Shirikisho  msimu wa 2025/26,...

Lissu aibwaga Jamhuri, kesi yahamia Mahakama ya Rufani

Na Mwandishi Wetu MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imekubali mapingamizi...