Serikali yatoa Bilioni 8 kujenga Kituo cha Umeme Imalilo-Simiyu

📌 Kituo cha Imalilo kukamilika Mei 2026, kuimarisha ubora wa umeme Bariadi

📌 Serikali yatoa Shilingi Bilioni 8 kugharamia mradi kwa asilimia 100

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme inayotekelezwa Mkoani Simiyu kwa lengo la kujionea maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Kupokea na Kusambaza Umeme cha Imalilo pamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 (220kV) kutoka Shinyanga hadi Simiyu.

Akizungumza mara baada ya ziara hiyo iliyofanyika tarehe 21 Februari 2026, Twange alisema mradi wa Kituo cha Imalilo ulianza kutekelezwa mwezi Oktoba 2025 na wataalamu wa ndani wa Shirika, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei 2026.

“Baada ya muda mrefu tumeanza kutekeleza mradi huu kupitia wataalamu wetu wa ndani ambapo tulianza mwezi Oktoba 2025, na tunatarajia kuukamilisha mwezi Mei 2026,” alisema Twange.

Alifafanua kuwa kwa sasa wananchi wa Bariadi wanategemea umeme kutoka mikoa jirani ya Shinyanga, Mwanza na Mara, hali inayosababisha kupungua kwa ubora wa umeme kutokana na umbali mrefu unaosafiri.

Alisema kukamilika kwa Kituo cha Imalilo kutaondoa changamoto hiyo na kuimarisha miundombinu ya umeme, hivyo kuhakikisha wananchi wa Bariadi wanapata umeme wa uhakika kuanzia Juni 2026.

“Kwa sasa wananchi wa Bariadi wanategemea umeme kutoka mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga, hali inayosababisha ubora wa umeme kupungua. Ujenzi wa kituo hiki utaimarisha miundombinu na kuondoa changamoto hizo kuanzia Juni 2026,” aliongeza.

Kwa sasa utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Kupokea na Kusambaza Umeme cha Imalilo umefikia asilimia 20.75.

Mradi huo unagharimu takribani Shilingi bilioni 8, fedha zinazofadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya kwanza.

spot_img

Latest articles

Simbu ang’ara tena Boston Marathon, ashika nafasi ya pili

Na Mwandishi Wetu Mwanariadha nyota wa Tanzania, Sajinitaji Alphonce Simbu, ameendelea kufanya vizuri Boston Marathon...

Tanzania mwenyeji Miss World 2027, Serikali yajipanga kuandika historia mpya duniani

Na Winfrida Mtoi TANZANIA imethibishwa rasmi kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa la urembo duniani ‘Miss...

Latra yatangaza nauli mpya za mabasi, daladala

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetoa bei mpya za nauli kwa...

Serikali yatoa neno vipaji vya kuogelea Afrika Mashariki vikichanua Dar

Na Winfrida Mtoi ​MASHINDANO ya kuogelea kwa watoto ya ‘East Africa Development Swimming Gala’ yameanza...

More like this