Nishati ya umeme inachochea kasi ya Maendeleo mkoani Singida- Meya Singida

📌Afungua kikao kazi kati ya TANESCO na viongozi wa Serikali za Mitaa, Kata na Madiwani

📌Aipongeza TANESCO kwa kuendelea kuboresha na kusogeza huduma zake kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Singida, Geofrey Mdama, amesema nishati ya umeme imekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma maendeleo na kuongeza kasi ya ukuaji wa mkoa wa Singida, kutokana na umuhimu wake katika kuimarisha fursa za kiuchumi, sekta ya viwanda, na uwekezaji.

Mstahiki Meya ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Februari 12, 2026, wakati akifungua kikao kazi kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenyeviti wa Serikali za Mitaa, watendaji wa kata pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Ameipongeza TANESCO kwa kutambua mchango wa viongozi hao, ambao ni ngazi muhimu katika kuwaelimisha wananchi kuhusu kazi zinazofanywa na Shirika hilo na umuhimu wa nishati ya umeme katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

“Naipongeza sana TANESCO kwa kutambua umuhimu na mchango wa viongozi hawa, kwa kuwa wanaishi karibu na wananchi. Kupitia wao, ni rahisi zaidi kuifikia jamii. Vilevile, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya umeme ambayo imekuwa na tija kubwa katika maendeleo ya nchi,” amesema Mdama.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Singida, Mha. Boniface Shitindi, amesema kikao kazi hicho kimelenga kuwapa elimu na kuwajengea uelewa viongozi hao juu ya shughuli zinazofanywa na TANESCO ili iwe rahisi kuifikisha elimu hiyo kwa wananchi kupitia mikutano yao.

Nao baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa, watendaji wa kata pamoja na madiwani wameeleza kuridhishwa na kikao hicho, hasa baada ya kuelimishwa kuhusu gharama za kuunganishiwa umeme, matumizi ya mita janja, umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya umeme, pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umeme ambayo ni nafuu zaidi.

Kikao hicho ni muendelezo wa vikao vinavyofanywa na Shirika hilo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhimu kuhusu maendeleo ya miradi ya umeme, maboresho yanayoendelea kufanyika, pamoja na elimu ya matumizi sahihi ya umeme.

spot_img

Latest articles

Waziri Gwajima aipongeza Tanesco kuandaa kongamano la wanawake la Nishati Safi ya kupikia

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima...

Makofi, vigelegele vimemrarua Mwigulu Nchemba?

Na Jesse Kwayu KATIKA mfumo wa utawala ambao chimbuko la madaraka ya dola ni wananchi,...

Katibu Mkuu Uwekezaji afanya ziara Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais – Uwekezaji, Dk. Fred Msemwa, leo...

DCEA yakamata Tani 9.93 za Dawa za Kulevya, Watuhumiwa 151 Watiwa Mbaroni

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata tani...

More like this

Waziri Gwajima aipongeza Tanesco kuandaa kongamano la wanawake la Nishati Safi ya kupikia

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima...

Makofi, vigelegele vimemrarua Mwigulu Nchemba?

Na Jesse Kwayu KATIKA mfumo wa utawala ambao chimbuko la madaraka ya dola ni wananchi,...

Katibu Mkuu Uwekezaji afanya ziara Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais – Uwekezaji, Dk. Fred Msemwa, leo...