Na Mwandishi Wetu
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha wadau wa Mahakama kilichofanyika leo Januari 22, 2026 Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilichoongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju kililenga katika kujadiliana juu ya uboreshaji wa utoaji wa huduma za Mahakama na Sekta ya Sheria kwa ujumla.



