Yanga yaikung’uta vibaya Mashujaa FC

Na Winfrida Mtoi

WANANCHI Yanga wameichakaza timu ya Mashujaa mabao 6-0, huku nyota mpya wa kikosi hicho Laurindo Aurelio maarufu Depu akitupia bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo Januari 19,2025 kwenye dimba la KMC Complex, jijini Dar es Salaam.

Depu raia wa Angola ni usajili mpya ndani ya kikosi cha Wananchi ambapo ameonekana kuanza vizuri kwani aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Maxi Nzengeli lakini alifanyikiwa  kufunga na kutoa pasi ya  bao.

Wachezaji wengine waliofunga katika mchezo huo ni Mohammed Damaro, Duke Abuya, Pacome Zouzoua, Prince Dube na Mudathir Yahya.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 19 na kuongoza msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa imecheza michezo saba ikishinda sita na kutoka sare mmoja, huku Mashujaa ikibaki nafasi ya tano na pointi 13 baada ya michezo 10.

Baada mchezo huo Wanajangwani hao wanajiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo wanatarajiwa kukutana na Al Ahly  nchini Misri, Ijumaa Januari 23,2025.

spot_img

Latest articles

Watumishi wapya wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wapigwa msasa

Na Mwandishi Wetu, Pwani OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH), kwa kushirikiana na Chuo cha...

Kituo cha kupoza umeme Mtera kuboresha upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua Kituo cha Kupoza...

Tanesco Kigamboni yatoa elimu y nishati safi ya kupikia shule ya msingi Malaika

Na Mwandishi Wetu KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati...

Dk. Nchimbi: Serikali imejipanga kuimarisha sekta ya uchukuzi

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema serikali imejizatiti kuhakikisha...

More like this