Tanesco Kigamboni yatoa elimu y nishati safi ya kupikia shule ya msingi Malaika

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, TANESCO Mkoa wa Kigamboni ilitoa elimu ya matumizi ya umeme kwa ajili ya kupikia katika Shule ya Msingi Malaika iliyopo Kigamboni.

Elimu hiyo ilitolewa wakati wa siku maalum ya ufunguzi wa shule, 13 Januari, 2026 (Back to School), iliyowakutanisha wazazi na walimu.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Kigamboni, Bi. Tumaini Mahwaya, alisema kuwa lengo la kutumia fursa hiyo ni kuhakikisha wazazi na waalimu wanapata uelewa wa kina kuhusu faida za kutumia nishati ya umeme kupikia akibainisha faida zake kuwa ni nishati salama, gharama nafuu na rafiki kwa mazingira.

“Shirika linakenga kuhakikisha wazazi na walimu wanaelewa kuwa kupikia kwa umeme ni salama, ni nafuu na kunalinda afya pamoja na mazingira. Tukibadili mtazamo wetu leo, tutakuwa tumewekeza kwenye maisha bora ya baadaye,” alisema Tumaini.

Vile vile, ili kuunga mkono utekelezaji wa matumizi ya nishati safi ya umeme katika taasisi za elimu, TANESCO ilikabidhi jiko la umeme aina ya Pressure Cooker lenye ujazo wa kilo 15 kwa uongozi wa shule hiyo ambalo litawarahisishia kupika shuleni hapo.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Malaika Bw. Ahmed Abdallah Fataki aliishukuru TANESCO Mkoa wa Kigamboni kwa msaada huo na kuahidi kulitumia kikamilifu, hatua itakayosaidia kuachana na matumizi ya nishati zisizo salama shuleni hapo.

“Jiko hili litatusaidia sana kuboresha huduma za chakula kwa wanafunzi na kutuondolea utegemezi wa nishati zisizo salama. Tunaishukuru TANESCO kwa kutukumbuka na kutuunga mkono katika ajenda ya nishati safi,” alisema Bw. Fataki.

Nao wazazi wa wanafunzi hao walionesha mwitikio mkubwa kwa kutembelea banda la TANESCO kupata elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuahidi kuacha matumizi ya nishati zisizo salama, ili kulinda afya zao na mazingira kwa ujumla.

spot_img

Latest articles

Kituo cha kupoza umeme Mtera kuboresha upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua Kituo cha Kupoza...

Dk. Nchimbi: Serikali imejipanga kuimarisha sekta ya uchukuzi

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema serikali imejizatiti kuhakikisha...

Wawili wajeruhiwa ajali ya moto Dar

Na Mwandishi Wetu WATU wawili wamejeruhiwa kutokana na ajali ya moto iliyotokea leo Januari 16,2025...

Tanzania yasisitiza uongezaji thamani madini barani Afrika

Riyadh, Saudi Arabia NAIBU Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa, amesema Tanzania imetambua shughuli za...

More like this

Kituo cha kupoza umeme Mtera kuboresha upatikanaji wa Umeme Iringa na Dodoma

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imezindua Kituo cha Kupoza...

Dk. Nchimbi: Serikali imejipanga kuimarisha sekta ya uchukuzi

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi amesema serikali imejizatiti kuhakikisha...

Wawili wajeruhiwa ajali ya moto Dar

Na Mwandishi Wetu WATU wawili wamejeruhiwa kutokana na ajali ya moto iliyotokea leo Januari 16,2025...