Na Mwandishi Wetu
MCHUNGAJI wa kanisa la National Christian Assembly Daudi Mashimo, amesikitishwa na kauli ya Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, iliyodai kuwa waliouwawa Oktoba 29, 2025 ni wengi kuliko waliouwawa kwenye vita vya Kagera.
Akizungumza na waandishi wa habari, mchungaji Mashimo alisema Hadi sasa hakuna chombo rasmi kilichotoa takwimu ya watu waliouwawa na kuhoji kiongozi huyo amepata wapi.
“Ametoa wapi takwimu hizo? Tunaomba sana tulipo tunahitaji amani na si kuvuruga wananchi? Alisema Jaji Mashimo.
Alisema Hadi sasa tume Bado inaendelea kufanya kazi iliyopewa Ili itoe majibu sahihi hivyo aliwataka viongozi kukaaa kimya na kungoja majibu ya tume.


