Mavazi ya kitamaduni kivutio kingine AFCON 2025

Na Winfrida Mtoi

SHAMRASHAMRA kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2025), zimezidi kupamba moto, hasa baada ya timu shiriki za michuano hiyo kuanza kuwasili nchini Morocco ambako yatafanyika mashindano hayo makubwa ya soka barani Afrika.

Mashindano hayo yayonatarajiwa kuanza Jumapili Desemba 21, 2025, yakishirikisha mataifa 24, yamekuwa kama fursa ya kipekee kwa baadhi ya nchi za Afrika kuonyesha utajiri wa tamaduni zao kupitia mavazi ya asili.

Kutokana na hilo mashindano hayo yanaonekana si kuhusu mpira pekee bali kuna vionjo vingi vinavyoyamba. Mashabiki wamekuwa wakivutiwa na hali hiyo, kwa mfano ukiangalia  jinsi  mataifa  mbalimbali kama vile Nigeria, Senegal, Mali, Benin  na Comoro walivyowasili Morocco ambapo wachezaji wao wameonekana wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni.

Hivyo aina hiyo ya mavazi inaonekana si urembo pekee bali ni utambulisho kimataifa unaoboresha taswira na sifa ya nchi, hali inayosaidia kuvutia watalii.

Afrika Magharibi wameonekana kuwa wazuri zaidi katika ubunifu wa mavazi yao ya kitamaduni  tofauti nan chi nyingine kama Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Angola na wengine ambao timu zao zimewasili zikiwa katika mavazi ya kawaida ya kimichezo.

Fainali hizo zinatarajiwa kuanza Jumapili Desemba 21, 2025, jumla ya mataifa 24 yakichuana ikiwamo Tanzania.

spot_img

Latest articles

Livembe: Mchakato wa Uchaguzi ulikuwa wa haki na halali

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe, amesema mchakato wa...

Sekta ya Viwanda na Biashara yazidi kutoa fursa kwa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema sekta ya viwanda...

Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na...

Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kwa AFCON 2025

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameiaga na...

More like this