Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameiaga na kuikabidhi bendera timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).
Hafla hiyo imefanyika nchini Misri ambako Taifa Stars ilikuwa kambini kujiandaa na mashindano hayo, kabla ya timu kuelekea Morocco kwa michuano hiyo inayotarajia kuanza Desemba 21.
Akizungumza wakati wa halfa hiyo, Prof. Kabudi, amekiahidi kikosi hicho ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vyema katika michuano hiyo mikubwa na yenye heshima kubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Aidha amewahimiza Watanzania kuipenda na kuipa moyo timu yao ya Stars kwa kuwashangilia na wale watakao kuwa na nafasi kwenda kujiunga nao kwenye mechi zao zote watakazocheza huko nchini Morocco.
Katika michuano hiyo Taifa Stars ipo kundi C lenye timu za Nigeria, Tunisia na Uganda, ambapo kikosi hicho kinachonolewa na kocha Miguel Gamondi mchezo wa kwanza kitakutana na Nigeria Desemba 21, 2025 Uwanja wa Fès Sports Complex, Morocco


