Mradi wa upanuzi Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Kinyerezi I Extension umekamilika

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema kuwa mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Kinyerezi 1 Extension umekamilika rasmi, ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa Transfoma yenye uwezo wa MVA 175.

Amesema hatua hii ni muhimu kwa kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa Jiji la Dar es Salaam, hususan maeneo ya Mbagala na Gongo la Mboto, ambayo yamekuwa yakikumbwa na changamoto za kukatika kwa umeme kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi.

Salome amesema hayo leo Desemba 11, 2025, wakati wa ziara yake katika vituo vya uzalishaji umeme vya Kinyerezi I, Kinyerezi II, Ubungo I, Ubungo II na Ubungo III akiongeza kuwa mradi tayari umeanza majaribio (testing).

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa. Transfoma zimefungwa, majaribio yanaendelea, na wananchi wa Gongo la Mboto na Mbagala sasa watapata umeme wa uhakika,” Salome.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema Shirika linaendelea kuboresha miundombinu yake ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka.

Amebainisha kuwa katika eneo la Kinyerezi kumefungwa Transfoma kubwa ya MVA 175, huku maeneo ya Gongo la Mboto na Mbagala yakiwekewa Transfoma ya MVA 120 ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya umeme.

Amesisitiza kuwa idadi ya watu imekuwa ikiongezeka Jiji la Dar es Salaam, hivyo miundombinu ya umeme lazima iboreshwe mara kwa mara ili kuendana na uhitaji uliopo.

“Lengo la Kinyerezi 1 Extension lilikuwa kuongeza uwezo wa kusambaza umeme unaozalishwa kuwafikia wateja wetu kwa kiwango kinachostahili,” amesema Twange.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...