Jeshi la Polisi latoa onyo wanaondelea kuhamasisha maandamano

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi nchini limesema  kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama  litaendelea kuimarisha hali ya usalama nchini na kulinda maisha ya wananchi na mali zao, huku likionya wale wanaondelea kuhamassha maandamano.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime leo Disemba 10, 2025, limeonya wale wanaopanga kujitokeza leo kwenye mitaa mbalimbali ili kufanya kile kinachoitwa maandamano ya amani kutokana na kushindwa kuyafanya jana Desemba 9, 2025.

“Jeshi la Polisi linaendelea kuwakumbusha, kuwasisitiza na kuwaonya wasifanye hivyo kwani wanachokiita maandamano ya amani yasiyo na kikomo yalipigwa marufuku kutokana na kukosa sifa kulingana na matakwa ya Katiba na sheria ya Polisi na Polisi wasaidizi sura 322,” amesema Misime.

Amesema kuwa  kwa atakayekaidi  kutii sheria za nchi kwa lengo la kuhatarisha usalama wa nchi ili kusimamisha shughuli za kiuchumi na kijamii zisiendelee, watadhibitiwa ili nchi ibaki salama na watanzania wema na wapenda amani wabaki salama.

Aidha taarifa hiyo imetoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya shughuli zao na kufuata maelekezo watakayokuwa wanapewa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo yote nchini sambamba na kutii sheria za nchi.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya...

More like this

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...