Na Mwandishi Wetu
BONDIA Debora Mwenda maarufu Bondia Mrembo, ameahidi kuiwakilisha vizuri Tanzania dhidi ya Mariam Dick kutoka Malawi watakapokutana katika pambano la Box on Boxing Day Desemba 26,2025, Warehouse Masaki Dar es Salaam.
Akizungumza leo Novemba 26, 2025, Debora amesema itakuwa mara yake ya kwanza kucheza pambano la kimataifa lakini anawaahidi watanzamia kuonesha mchezo mzuri na kuibuka na ushindi wa kishindo.
“Nashukuru kwa nafasi hii niliyoipata, ya kuonesha kitu nilichonacho, nimejiandaa vyakutosha nataka kuwaonesha watanzania kuwa najua kuufanya mchezo huu hata zaidi ya mwanaume,”
Amesema hana woga wowote kwa sababu amewekeza nguvu zake zaidi katika mazoezi na kila siku zinavyokwenda anazidi kuwa bora.
Naye mwalimu wa bondia huyo, Dickson Tembo amesema, anaendelea na mazoezi ya kibabe,hivyo watanzania wajiandae kushangilia ushindi wa kishindo siku hiyo.


