Na Winfrida Mtoi
Simba imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kufungwa na Petro de Luanda bao 1-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijjni Dar es Salaam.
Matokeo hayo yamewafanya mashabiki wa timu hiyo waliojitokeza kwa wingi kuondoka kwa unyonge uwanjani wakiwa hawaamini kilichotokea.
Wikiendi ijayo Simba itakuwa ugenini nchini Mali kuikabili Stade Malien ambayo jana ilitoka suluhu na Esperance ya Tunisia.

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC wameanza vibaya hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kufungwa ugenini mabao 2-0 na AS Maniema ya DR Congo.
Kati ya wawakilishi wanne wa Tanzania katika michuano hiyo ya CAF yaani Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la. Shirikisho, Yanga pekee ndio imeanza vizuri kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FAR Rabat ya Morocco, wakati Singida Bs ikipoteza ugenini kwa kufungwa 2-0 na CR Belouizdad


