Na Winfrida Mtoi
BAO pekee lililofungwa na Prince Dube dakika ya 58, limeipa Yanga alama tatu muhimu katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi AS FAR Rabat.
Ushindi huo wa bao 1-0, walioupata Wanajangwani hao kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar unaifanya timu kuingia katika mchezo wa pili na matumaini ya kuendelea kufanya vizuri.
Yanga inayonolewa na kocha raia wa Ureno, Pedro Goncalves, itacheza mechi ya pili ya michuano hiyo ugenini Ijumaa ijayo dhidi ya JS Kabylie ya nchini Algeria.

Katika hatua nyingine mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize amepokea tuzo yake ya bao bora Afrika mwaka 2025 iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Novemba 19,2025 nchini Morocco.
Mzize alishindwa kwenda Morocco kuhudhuria halfa ya utoaji tuzo hizo kutokana na hali yake ya kiafya.


