Na Mwandishi Wetu
Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ amefariki dunia leo, Novemba 16,2025.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Ernest Ibenzi amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa MC Pilipili amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia.


