Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, kutokana na sababu za kiusalama.

Leo Novemba 10, 2025 Lissu alitarajiwa kufikishwa  katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, wakisaidiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, kwa ajili ya kusikilizwa kwa shahidi wa nne wa upande wa Jamhuri kutoa ushahidi wake dhidi ya kiongozi huyo wa Chadema.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Thawabu Issa, aliieleza mahakama kuwa walifika mahakamani na  kugundua kwamba mshtakiwa hakuwepo, hivyo kufanya  jitihada za kuwasiliana na Mkuu wa Gereza kujua sababu za kutokuwepo kwake.

“Tulipofika hapa tulikuta mshtakiwa hayupo. Tulifanya jitihada za kuwasiliana na Mkuu wa Gereza na tukaelezwa kwamba wameshindwa kumfikisha kwa sababu za kiusalama,” amesema Wakili Issa.

Upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama kuhairisha kesi hiyo kwa siku 14, lakini katika maamuzi yake Mahakama kupitia Jaji Danstan Ndunguru ikatoa maelekezo kuwa shauri hilo linaahirishwa hadi Jumatano na si kwa siku 14 kama ilivyoombwa na Jamhuri. Huku akisisitiza  kuwa mshtakiwa  pamoja na wafikishwe makahamani ili shauri liendelee.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

More like this