Na Mwandishi Wetu
Bondia Mtanzania Zulfa Macho amemchapa kwa pointi Bisambu Deborah wa DR Congo katika pambano la nusu fainali ya mashindano ya ngumi ya Kanda ya Tatu Afrika, yanayoendelea Nairobi, Kenya.
Ushindi huo umemfanya Zulfa kulipa kisasi kwa bondia huyo ambaye mwaka 2024 alimpiga a kwa pointi 3-2 dhidi katika Mashindano ya Afrika yaliyofanyika Kinshasa, DR Congo.
Katika mchezo wa fainali Zulfa anayechezea uzito wa kilo 54(Bantamweight), atakutana na Amina Martha kutoka Kenya Ijumaa Oktoka 24,2025.
Martha ni mshindi wa medali katika mashindano ya Mataifa ya Afrika (African Games) yaliyofanyika Accra, Ghana 2024.