Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Simba imeteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kuwania tuzo ya Klabu Bora Afrika (Club of the Year) kwa mwaka wa mashindano wa 2025.
Simba imeingia katika mchujo wa kuwania tuzo hiyo ikichuana na timu 10 ambazo ni Cr Belouizdad, Constantine, Al hilal Omdurman, Zamalek, Stellenbosch, Rs Berkane, Mamelod Sundwons, Orlando Pirate, Pyramids pamoja na Asec Mimosas.

Kwa upande wa wachezaji, Nahodha wa klabu ya Simba, Shomari Kapombe ametajwa kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa klabu kwa Afrika kwa mwaka 2025.
Wachezaji wanaochuana nao ni Fiston Kalala Mayele (Pyramids FC), Ismail Belkacemi (Al Ahli ya Libya), lbrahim Blati Touré(Pyramids), Issoufou Dayo( aliyekuwa RS Berkane) na Emam Ashour (Al Ahly), Ibrahim Adel(aliyekuwa Pyramids), Mohamed Hrimat (AS FAR Rabat), Mohamed Chibi (Pyramids) na Oussama Lamlioui (RS Berkane).