Na Mwandishi Wetu
Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz.
Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya kupoteza mchezo kwa kufungwa ugenini na Silver Strikers bao 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa usiku huu, timu itakuwa chini ya Kocha Msaidizi Patrick Mabedi, huku mchakato wa kumtafuta mwingine ukiendelea.
Folz raia wa Ufaransa alijiunga na Wanajangwani hao, Julai, 2025 akitokea klabu ya Olympique Akbou ya Algeria ambako alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi.
Kocha Romuald Rakotondrabe kutoka Madagascar anatajwa kuwa ndiye atakayechukua nafasi ya Mfaransa huyo.