Bulugu awahamasisha Wafanyakazi Kiwanda cha Kahawa Mbozi kumpigia kura Dkt. Samia

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Msaidizi Mkuu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM, Bulugu Magege, leo 30/09/2025 amekutana na wafanyakazi wa Mbozi Coffee Curing Company Limited na kuwasisitiza wajibu wao wa kizalendo wa kumpa kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea wa CCM katika nafasi za Ubunge na Udiwani.

Katika mazungumzo hayo, Bulugu aliwaeleza kuwa Dkt. Samia ni Kiongozi mwenye upendo na watanzania anayejali wakulima na wafanyakazi kwa kuendeleza sekta ya kilimo na viwanda hususani kahawa, ambayo ni uti wa mgongo wa wananchi wa Mbozi na mkoa mzima wa Songwe. Alisisitiza kuwa kura zao kwa Dkt. Samia ni kura za maendeleo ya kweli kwa taifa.

Katika ziara hiyo, Bulugu aliambatana na Haji Shabani Mwalimu, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbozi na Noel Donald Mkwemba, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa Songwe.

Wote kwa pamoja waliwaeleza wafanyakazi hao kuwa CCM ni chombo pekee cha kuwaletea mustakabali bora na kuwataka watimize ahadi yao ya kumpa ushindi wa kishindo Dkt. Samia ifikapo Oktoba 29, 2025.

spot_img

Latest articles

Oktoba 29 siku ya giza, ifungue milango ya haki

OKTOBA 29, 2025 itabakia kuwa siku ya giza na machungu katika historia ya Jamhuri...

Fountain Gate yatoa kocha bora

Na Mwandishi Wetu Kocha wa timu ya Fountain Gate,  Mohamed Laizer amechaguliwa kuwa kocha bora...

Nyota JKT Queens aipigia hesabu Asec Mimosa

Na Winfrida Mtoi Mshambuliaji wa JKT Queens FC, Jamila Rajabu, amesema  amejipanga  kutengeneza  nafasi na...

Zungu achaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Mwandishi Wetu MBUNGE mteule wa Jimbo la Ilala Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi...

More like this