Bulugu awahamasisha vijana wa Mlowo kuichagua CCM

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Msaidizi Mkuu Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa CCM, Bulugu Magege, leo tarehe 30/09/2025 amekutana na vijana wa Kata ya Mlowo na kuwasisitiza kuhakikisha kura zao zote wanampa Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wa CCM katika ngazi zote.

Katika mazungumzo hayo, Bulugu aliwaeleza vijana kuwa Ilani ya CCM imewapa kipaumbele kikubwa vijana ikiwemo mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri, ajira, elimu bora na uwezeshaji kiuchumi.

Alisisitiza kuwa Dkt. Samia ni Rais mwenye upendo mkubwa kwa vijana, anayetamani kuwaona wakibadilisha maisha yao kupitia fursa alizozileta.

Bulugu aliambatana na Haji Shabani Mwalimu, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Mbozi na Noel Donald Mkwemba, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mkoa wa Songwe.

Vijana wa Mlowo walimhakikishia kuwa wako tayari kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo ifikapo Oktoba 29, 2025.

spot_img

Latest articles

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

More like this