Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Japan Bank for International Cooperation (JBIC) pamoja na Japan International Cooperation Agency (JICA) zimeahidi kushirikiana na Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umeme (ETDCO) katika utekelezaji wa miradi yake ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini Tanzania, ikiwemo uwekezaji wa kimkakati.

Wakizungumza katika vikao kazi vilivyofanyika, jijini Tokyo, Japan, viongozi kutoka JBIC na JICA wameeleza dhamira yao ya kushirikiana na ETDCO katika nyanja za uwekezaji, uhamishaji wa teknolojia na utekelezaji wa miradi ya Nishati nchini Tanzania itakayo saidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa Nishati ya umeme.
Vikao kazi hivyo ni mwendelezo wa mafanikio ya ETDCO katika Maonesho ya Dunia (Expo 2025) yanayofanyika Osaka, Japan, ambapo Kampuni hiyo inaendelea kujitangaza kimataifa na kuimarisha mtandao wa ushirikiano kwa ajili ya kuharakisha utekelezaji wa miradi yake.
