Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemteua Oscar Mirambo kuwa Kaimu Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Kidao Wilfred.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 24, 2025 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, mkataba wa Kidao unafikia tamati Septemba 30 mwaka.
“Uteuzi wa Mirambo ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, utaanza rasmi tarehe 1 Oktoba 2025,” imesema taarifa hiyo.

Kidao amedumu katika nafasi hiyo miaka nane, kwa mara ya kwanza aliteuliwa mwaka 2017, hivyo kukaa kwenye kiti hicho kwa mihula mitatu tofauti ya uongozi wa Rais wa TFF, Wallace Karia.