Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali waridhishwa na kasi ya utekelezaji Bwawa la Kidunda

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wametembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda, mkoani Morogoro huku wakisema wana nafasi ya kushauri na kusaidia mambo mbalimbali yakiwemo ya kimkataba.

Mradi wa Kidunda unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 335, unatarajia kukamilika ifikapo Juni 2026 na kuchangia kuimarisha huduma ya maji mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, kuzalisha umeme megawati 20 ambazo zitaunganishwa katika gridi ya taifa.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kisamo Fredrick ameongoza ujumbe wa ofisi hiyo kutembelea mradi huo akisema, wao wana nafasi kubwa katika miradi ya kimkakati na kimaendeleo kushauri na kusaidia mambo mbalimbali yakiwemo ya kimkataba ili kuhakikisha miradi inakwenda bila kukwama.

“Niwashukuru DAWASA, wamekua wakitushirikisha mara kwa mara, nafasi yetu ni kupitia maswala mbalimbali katika miradi na kuzuia changamoto zinazoweza kukwamisha miradi kutokea na kusaidia kusukuma miradi iweze kukamilika kwa wakati,” amesema Kisamo.

Amesema changamoto zilizobainishwa katika utekelezaji wa mradi huu wamezipokea na kwa nafasi yao watashirikiana na wizara zinazohusika kuhakikisha mradi huu haukwami ili uweze kuleta tija.

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi kutoka DAWASA, Mhandisi Christian Christopher ameshukuru ujumbe huo kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutembelea na kusikiliza changamoto zinazokabili.

“Ukaribu wao kwetu ni muhimu sana kwani wanatusaidia kubaini viashiria mbalimbali vinavyoweza kuleta shida na kufanya mradi usitekelezeke kwa wakati. Haya yote waliotushauri tunayapokea kwa uzito mkubwa na kuanza kuyafanyia kazi mara moja,” amesema Mhandisi Christopher.

spot_img

Latest articles

Ofisi ya Msajili wa Hazina yatoa wito wa utawala bora kuimarisha uwekezaji wa umma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) imesisitiza kuwa mustakabali wa mafanikio...

TTB yamkaribisha bingwa wa Masumbwi duniani Terence kwa ziara ya utalii

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amemkaribisha nchini...

DAWASA yasisitiza matumizi ya bidhaa za ndani kuimarisha huduma ya maji

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)...

DCEA yateketeza kilo 504.36 za Heroin Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara MAMLAKa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza...

More like this