Ahukumiwa kufungo  cha  miaka 20 jela kwa shambulio la aibu kwa mtoto

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Agosti 18, 2025 imetoa hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa mtuhumiwa Idd Shelugwaza (26), mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kwakibuyu, Kata ya Kipumbwi, wilayani Pangani, baada ya kupatikana na hatia ya kosa la shambulio la aibu dhidi ya mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Awali, ilielezwa mahakamani kuwa mnamo Juni 24, 2025 huko Kijiji cha Kwakibuyu, mtuhumiwa alitenda kosa hilo dhidi ya mtoto huyo  ambaye ni mwanafunzi na mkazi wa kijiji hicho. Tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Pangani ambapo mtuhumiwa alikamatwa  na uchunguzi wa shauri hilo ulianza mara moja.

Shauri hilo lilifunguliwa mahakamani kwa namba 15855/2025 na kupelekwa mbele ya Hakimu Francisca Magwiza – SRM. Baada ya kusomewa shtaka, mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo, na shauri liliendelea kwa mashahidi mbalimbali kutoa ushahidi wao mahakamani.

Akisoma hukumu jana Agosti 18, 2025, Hakimu Magwiza alisema kuwa mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, hivyo kumpata mtuhumiwa na hatia ya shambulio la aibu na kumhukumu kifungo cha miaka 20 jela ili iwe fundisho kwa jamii na kulinda haki za watoto.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this