Yanga yafuta taarifa ya ufafanuzi wa milioni 100, Chadema yawajia juu viongozi wa klabu

Na Mwandishi Wetu

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka viongozi wa klabu ya  Yanga, kutathmini uhalali wao wa kuongoza klabu hiyo kwa kitendo cha kukichangia Chama Cha Mapinduzi (CCM)  sh 100 milioni.

Taarifa ya Chadema iliyotolewa leo tarehe 15 Agosti 2025, na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa  Chadema, Brenda Rupia.

Katika taarifa hiyo Rupia ameeleza kuwa kitendo cha Yanga kuichangia CCM ni dharau kwa wanachama na mashabiki wenye itikadi za vyama mbalimbali za siasa.

Rupia ameeleza kuwa taarifa ya yanga ya kudai kuwa mchango huo ulitoka kwa GSM haikuwa ya kweli kwa kuwa taarifa za awali zilidai kuwa GSM, amechangia sh.10 Bilioni, huku Yanga ikichangia sh.100 milioni.

Katika hatua nyingine Yanga imeondoa katika mitandao yake ya kijamii  taarifa ya ufafanuzi waliyoandika kwa Umma jana juu ya mchango huo, pamoja na kuwaomba radhi mashabiki waliyoitoa jana Agosti 14,2025.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA KUZINDUA RASMI MRADI WA JNHPP AGOSTI 22, 2026

📌Waziri Ndejembi asema ni tukio la kihistoria litakaloshuhudiwa na watanzania pamoja na wageni 📌Asema...

JAJI MSHIBE ASISITIZA MAANDALIZI YA KISEKTA KATIKA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya...

More like this