Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Yanga imewaomba radhi mashabiki wake na kutoa kuhusu fedha kiasi cha sh 100 milioni walizotoa mchango katika harambee ya kuchangia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kufanikisha kampeni za Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29,2025.
Yanga imeomba radhi katika taarifa yake iliyotoa kwa Umma leo Agosti 14, 2025 baada ya mashabiki wake kuja juu mitandaoni wakiibua mijadala wakihisi fedha zilizotumika ni za wanachama.
Katika taarifa hiyo imefafanua kuwa fedha za mchango kwa CCM Agosti 12, 2025 zimetoka katika Taasisi ya GSM Foundation iliyopo chini ya mfadhili wa klabu hiyo, Ghalib Said.
