VETA yajipanga kushirikiana na Toyota Tanzania kuimarisha mafunzo ya ufundi magari

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepanga kuimarisha ushirikiano wake na Kampuni ya Toyota Tanzania Limited ili kuboresha mafunzo ya ufundi magari, hususan kwa wakufunzi na wanafunzi wa vyuo vya VETA nchini.

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Menejimenti ya VETA Makao Makuu ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, na kuwahusisha Menejimenti na wataalam kutoka VETA Makao Makuu, Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam na walimu kutoka vyuo vya Dar es Salaam na Pwani, iliyofanyika jana Agosti 12,, 2025, katika ofisi na karakana za Toyota Tanzania, jijini Dar es Salaam.

CPA Kasore amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza kuhusu mifumo ya matengenezo ya magari yanayofanywa na Toyota, teknolojia mpya sokoni, na namna kampuni hiyo inavyowawezesha mafundi kuwa mahiri katika kazi zao.

Pia ameweka wazi dhamira ya VETA kushirikiana na Toyota katika kutoa mafunzo ya kuongeza umahiri kwa wakufunzi na wanafunzi wanaojifunza fani zinazohusiana na magari.

“Magari ya Toyota yanatumika kwa kiwango kikubwa nchini, hivyo ni muhimu wakufunzi na wanafunzi wetu wawe na uelewa wa kina ili wafanye matengenezo bora wanapoingia kazini,” amesema CPA Kasore.

Meneja Mkuu wa Toyota Tanzania, Kadiva Noah William, ameipongeza VETA kwa hatua hiyo akisema, “VETA mnazalisha tunachokitumia (mafundi) na sisi tunatoa huduma mnayoitumia (magari na matengenezo), hivyo tunategemeana.”.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shughuli za Usambazaji wa Toyota, Stanley Joseph, amesema ushirikiano huo utarahisisha utoaji wa mrejesho wa utendaji wa wahitimu wa VETA sambamba na kufuatilia mabadiliko ya teknolojia, ikiwemo magari yanayotumia gesi na mafuta.

Mkufunzi wa Toyota Tanzania, Michael Mruma, ameeleza kuwa kampuni hiyo ina chuo maalum kinachotoa mafunzo ya ufundi na stadi laini kwa mafundi, yakiwemo umakenika, umeme wa magari, urekebishaji bodi, huduma kwa wateja, usimamizi wa vifaa na mbinu za Kaizen.

Amesisitiza umuhimu wa mafundi kuwa na ujuzi wa pamoja wa umakenika na umeme wa magari ili kubaini matatizo kwa haraka, jambo ambalo kwa sasa linatolewa kama fani tofauti katika vyuo vya VETA.

Katika mazungumzo hayo, pande zote ziliona haja ya kurasimisha ushirikiano ili mafunzo yanayotolewa katika vyuo vya ufundi stadi yaendane na uhalisia wa soko la ajira, pamoja na kuinua viwango vya wakufunzi.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...