Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Tume Huru yaTaifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, amemkakabidhi Georges Busungu.
mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha rais na makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA).
Mgombea huyo aliambatana na mgombea mwenza, Ali Makame Issa leo Agosti 11, 2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.
