Sangweni: Sekta ya gesi asilia, Kilimo zinategemeana

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkundo wa Juu wa Petroli (PURA), Mha. Charles Sangweni amesema kuwa sekta ya gesi asilia na sekta ya kilimo ni sekta zinazotegemeana kwa karibu na kwamba sekta hizi zikifungamanishwa vizuri zitaongeza tija katika uchumi.

Sangweni ameyasema hayo Agosti 07, 2025 alipotembelea Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane yanayoendelea Jijini Dodoma.

Sangweni amebainisha kuwa, gesi asilia inayozalishwa nchini inaweza kutumika kama malighali kuzalisha ammonia, kemikali ambayo hutumika kuzalisha mbolea za aina mbalimbali ikiwemo urea.

Ameeleza pia kuwa, matumizi ya gesi asilia kwenye magari yamesaidia kupunguza gharama za uendeshaji hivyo gesi asilia ikitumiwa katika magari yanayosafirisha mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi itasaidia kupunguza gharama za usafirishaji.

Kwa upande mwingine, Sangweni ameeleza kuwa sekta ya kilimo imeendelea kuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa miradi ya mafuta na gesi asilia kwa kulisha wataalamu wanaofanya kazi katika miradi ya mafuta na gesi asilia nchini.

Pamoja na sekta ya kilimo kutoa huduma hii muhimu, Sangweni amesema bado kumekuwa na changamoto kadhaa ikiwemo kampuni hususan kampuni za nishati za kimataifa kuhitaji bidhaa za kilimo zenye ubora na viwango ambavyo watoa huduma wachache wakitanzania wanakidhi.

Hata hivyo, Sangweni amebainisha kuwa, PURA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa viwango na ubora hitajika vinafikiwa kwa maslahi mapana ya uchumi.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...