Mhandisi Mramba afungua mafunzo ya Teknolojia ya Nishati Jua kwa wataalam

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba amefungua mafunzo ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali nchini yanayohusu usanifu, utengenezaji na ufungaji wa mifumo ya Nishati ya Jua na matumizi yake.

Matumizi hayo ni kuchemsha, kupika, kupoza maji pamoja na kukausha mazao kwa kutumia nishati ya Jua.

Akifungua mafunzo hayo jijini Dar es Salaam, Mhandisi Mramba amesema mafunzo kuhusu teknolojia ya nishati ya Jua yanaenda sambamba na vipaumbele vya taifa katika Dira 2050 ambapo Dira hiyo inagusia mikakati ya kuendeleza matumizi ya nishati jadidifu nchini.

“Nishati Jadidifu ikiendelezwa kikamilifu itakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi, itapunguza utegemezi katika nishati isiyosafi ikiwemo kuni na kuongeza upatikanaji wa huduma za nishati kwa njia ya kisasa zaidi” amesema Mhandisi Mramba.

Mramba amewaasa washiriki wa mafunzo hayo kuwa makini na kuzingatia kile kinachofundishwa ili kiweze kuleta tija nchini.

Vilevile, Mhandisi Mramba ameeleza kuwa Tanzania inajivunia ushirikiano wake na mashirika mbalimbali ya Kimataifa katika kuendeleza Sekta ya Nishati ikiwa ni pamoja na kufanikisha mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo wataalam.

Mafunzo hayo ya Nishati ya Jua yanayojulikana kama SOLTRAIN + yameandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Kituo Mahiri cha Matumizi Bora ya Nishati na Nishati Jadidifu (SACREEE) ambacho kipo chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika (SADC).

Jumla ya washiriki 40 kutoka taasisi mbalimbali wanahudhuria mafunzo hayo ya siku mbili wakiongozwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.

spot_img

Latest articles

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this