Mfanyabiashara ahukumiwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka minne

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Wilaya ya Mbozi imemtia hatiani na kumhukumu kifungocha maisha gerezani, mfanyabiashara Athuman Mtibwa (35) na kulipa kiasi cha fidia milioni moja kwa mwathirika kwa kosa la kubaka mtoto wa miaka minne.

Kwa mujibu wa taarifa iliyokwa kwenye mtandao wa kijamii  @polisi.tanzania  Mtimbwa alikamatwa Oktoba 21, 2024 maeneo ya kiwandani Mlowo, Wilaya ya Mbozi, ilielezwa mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitekeleza tukio hilo la ubakaji kwa kumvizia mwanafunzi huyo wa darasa la awali akiwa anatoka shule na kumvuta kwa nguvu kisha kumuingiza katika kibanda chake cha biashara na kumbaka.

Akitoa hukumu hiyo Julai 29, 2025 kesi namba 32392 ya mwaka 2024, Hakimu mkazi wa Wilaya ya Mbozi,Nemes Chami alisema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

“Mshtakiwa amehukumiwa kifungo pamoja na fidia hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto,”

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this