Na Winfrida Mtoi
Bao pekee la Shomary Kapombe dakika ya 89, limeipa ushindi wa 1-0 Taifa Stars dhidi ya Mauritania katika mchezo wa michuano ya CHAN kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Ushindi huo wa Stars unakuwa wa pili mfululizo baada ya mechi iliyopita ya ufunguzi wa michuano hiyo kushinda 2-0 dhidi ya Burkina Faso.
Taifa Stars inaongoza kundi B baada ya kufikisha pointi 6 na kujiweka nafasi nzuri ya kutinga robo fainali.