Maendeleo ya elimu ni mkombozi wa Taifa lolote duniani- Majaliwa

Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maendeleo katika sekta ya elimu ni mkombozi na mafanikio ya Taifa lolote duniani.

Amesema kwa kutambua hilo, uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan uliamua kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora katika ngazi zote.

Amesema hayo wakati alipozungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Lucas Malia iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2025.

“Mliopo shuleni na mnaokuja, tambueni kuwa tuna maeneo muhimu ya kuwaelimisha, mtapata elimu iliyobora na imara itakayowapa maarufa na ujuzi ili muweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi,”amesema.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho ya mitaala kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo duniani ikiwemo mahitaji makubwa ya ajira kwa vijana.

“Mabadiliko haya yameifanya mitaala yetu itakayofundishwa shuleni kila mwanafunzi akimaliza ana uwezo wa kutumia mazingira alimo na taaluma aliyonayo kuyabadilisha kuwa uchumi”

Akisoma matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2025, Makamu Mkuu wa Shule Amon Chalamila hiyo amesema kuwa shule hiyo ilisajili wanafunzi 188 ambapo wote walifanya mitihani na wanafunzi 90 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 95 walipata daraja la pili, wanafunzi watatu walipata daraja la tatu na hakuna mwanafunzi aliyepata daraja na nne na sifuri. “Ufaulu huu ni sawa na GPA ya 2.34”.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...