Job Ndugai afariki Dunia

Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai amefariki dunia leo Agosti 6,2025 akiwa akiwa anapatiwa  matibabu hospitalini baada ya kuugua ghafla.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, imethibitisha Ndugai kufariki ambapo Spika wa Bunge  Dk. Tulia Ackson amtoa pole  kwa familia na wananchi wa  Jimbo la Kongwa.

“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasia mkongwe na Spika  Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea lei jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu na jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu”, amesema Dk Tulia.

Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni.

Ndugai ambaye amezaliwa January 22,1960 alishinda kura za maoni za Ubunge wa Jimbo la Kongwa kwa kupata kura 5690.

spot_img

Latest articles

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

Viongozi wa dini waendelea kihimiza amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha...

More like this