DC Mkalama avutiwa VETA, ahamasisha wananchi kujitokeza kupata ujuzi

Na Tatu Mohamed

MKUU wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali ametoa wito kwa wananchi wa rika zote, kujitokeza kwa wingi kupata mafunzo ya ujuzi yanayotolewa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), akisisitiza kuwa taasisi hiyo ni njia ya uhakika ya kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa.

Akizungumza wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya Wakulima na wafugaji (Nanenane) yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, Machali amesema ameshuhudia mafanikio ya moja kwa moja kwa vijana na wanawake waliopata mafunzo ya ufundi na ujasiriamali kupitia VETA.

“Nimepita hapa VETA naona kabisa kuna watu waliowezeshwa. Wanawake na vijana wamejifunza kuchakata bidhaa za kilimo na kuziongezea thamani. Wapo wanaotengeneza sabuni, juisi, biskuti, na bidhaa nyingine nyingi,” amesema.

Ameongeza kuwa mafunzo yanayotolewa na VETA ni ya vitendo na hujikita katika kumpa mtu ujuzi wa moja kwa moja unaoweza kumpatia kipato, hivyo kuwataka wananchi kutokupuuza fursa hiyo muhimu.

“Wito wangu kwa wananchi, hata sisi wakubwa, twendeni VETA. Si kwa ajili ya cheti tu, bali kwa ajili ya kujifunza ujuzi wa maisha. VETA wanakupa ujuzi wa moja kwa moja, unajifunza kutengeneza bidhaa, kuchakata vyakula, hata ufundi stadi mbalimbali,” amesisitiza Machali.

Aidha, amewapongeza viongozi na wakufunzi wa VETA kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwainua wananchi kupitia elimu ya ufundi, huku akizitaka halmashauri na wadau wengine wa maendeleo kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo ili kufikia watu wengi zaidi.

Maonesho ya Nanenane yamekuwa jukwaa muhimu kwa VETA kuonesha kwa vitendo mafanikio ya elimu ya ufundi, na mwaka huu yameendelea kuonesha jinsi elimu hiyo inavyoweza kubadili maisha ya wananchi kwa kutoa suluhisho la ajira na kuongeza tija katika sekta ya kilimo na viwanda.

spot_img

Latest articles

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this