Na Mwandishi Wetu
Msanii wa Bongofleva, Abdulaziz Abubakar ‘ Dogo Janja’, ameongoza katika kura za maoni ya udiwani katika Kata Ngarenaro, mkoani Arusha kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Akitangaza matokeo hayo leo Agosti 4, 2025, msimamizi wa uchaguzi huo Sofia Islam amesema Dogo Janja amepata kura 76, Isaya Doita alipata kura 60 na Benjamin Mboyo kura mbili.
Kura za maoni kwa wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kupitia CCM zinafanyika nchini leo kote.