Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi Wilaya ya Babati mkoani Manyara limewataka vijana kuacha tabia ya kukaa vijiweni na kucheza pool table asubuhi badala yake wajishughulishe na kazi halali za kujipatia kipato ili kuepuka kujiingiza katika matukio ya uhalifu
Wito huo umetolewa na Polisi Kata ya Duru Wilaya ya Babati, Mkaguzi wa Polisi Fadhil Mgeta , Julai 21, 2025 wakati akitoa elimu ya madhara ya kukaa kijiweni bila kufanya kazi kwa vijana katika Kijiji cha Qatadium Kata ya Duru.
Pia ametoa onyo kwa vijana hao kuacha kujihusisha na matukio ya uhalifu kwani ni kosa la jinai na Jeshi la Polisi halitavimilia mtu au watu watakaobainika.