Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha Kimataifa cha Sheria za Biashara na Uwekezaji

Na Mwandishi Wetu

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari ameshiriki kikao cha 58 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Sheria za Biashara na Uwekezaji kinachofanyika kwa siku 2 kuanzia tarehe 21 hadi 22 Julai, 2025 Jijini Vienna, Austria.

Kikao hicho pamoja na mambo mengine kilijadili taratibu za Utatuzi wa Migogoro kati ya Wawekezaji na Serikali katika Mikataba ya Mataifa.

Kikao hicho pia kilijadili mageuzi yanayokusudiwa kufanywa katika Sheria za Kimataifa za biashara. Mageuzi yanayopendekezwa ni pamoja kuhakikisha Sheria za Biashara za Kimataifa zinajali maslahi ya mataifa yanayoendelea, Tozo na gharama zinazotolewa na Mabaraza ya Kimatifa zina uhalisia, Kuwepo kwa uwazi na ufanisi katika mwenendo wa Mashauri, na Kuwepo na uwezekano wa kukata rufaa kwenye maamuzi ya mabaraza ya Usuluhishi ya Kimataifa.

Kupitia kikao hicho Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuweka taratibu za kushughulikia malalamiko ya wawekezaji mapema kabla haijawa migogoro (Mechanisms for prevention of Disputes).

Aidha, Tanzania kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kuwa mstari wa mbele kuchochea mageuzi kwenye utatuzi wa migogoro ya uwekezaji, kwa kusisitiza uwepo wa njia mbadala za utatuzi wa migogoro ikiwemo kutumia njia za upatanishi (amicable settlement).

Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametembelea Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania nchini Austria na kupokelewa na Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania nchini Austria Gerald Mbwafu, ambapo amemshukuru kwa mapokezi mazuri na kufanikisha ujumbe wa Tanzania kuhudhuria kikao hicho.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

More like this