Madai ya dada wa Polepole kubebwa, Polisi yachunguza 

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limesema limepokea taarifa za kuchukuliwa na watu asiowafahamu na  kurejeshwa  kwa mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Christina  Polepole, mwenye umri wa miaka 52, mkazi wa Bahari Beach, mtaa wa Katumba, Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo  Julai 18,2025 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro tukio hilo lilianza kuripotiwa kupitia mitandao ya kijamii mnamo Julai 17, 2025, ambapo mtu aliyejitambulisha kwa jina la Humphrey Polepole akijieleza kuwa  dada yake alichukuliwa na watu wasiojulikana waliovamia nyumba yake kwa kuruka ukuta.

“Dada huyo alifika mwenyewe katika kituo cha Polisi Kawe na kutoa taarifa  kuwa jana  alichukuliwa  na watu ambao hakuwafahamu na baadae walimrudisha nyumbani kwake jana hiyo hiyo,” ameeleza Muliro.

Jeshi hilo limethibitisha kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo kwa kushirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya usalama, huku likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za uchunguzi zikiendelea.

Aidha Kamanda Muliro amesema kwa kushirikiana na wananchi Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha usalama katika jiji la Dar es Salaam.

spot_img

Latest articles

Rostam aanika maono yake umiliki mpya ya NMG

Na Mwandishi Wetu MFANYABIASHARA na mwekezaji wa Tanzania, Rostam Azizi, ametangaza uwekezaji mkubwa wa kimkakati...

Tanzania Kunufaika na Mradi wa Umoja wa Ulaya wa Kukabiliana na Hatari za Sumu za Kemikali

Na Mwandishi wetu TANZANIA iko katika hatua za awali za upembuzi wa kushiriki katika mradi...

Rostam Aziz ainunua Nation Media ya Kenya

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taarifa Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz imeingia makubaliano ya...

Mwili wa Mwanahabari Mkongwe Makaranga waagwa Dar, kuzikwa Mwanza

Na Mwandishi Wetu WAANDISHI wa Habari, Wahariri, ndugu na jamaa leo Machi 10, 2026, wamejumuika...

More like this