Vyombo vya Habari Vatajwa Kuwa Nguzo Muhimu Katika Mapambano Dhidi ya Dawa Bandia

Na Tatu Mohamed

MKUU wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, amesema kuwa vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kuhakikisha jamii inalindwa dhidi ya matumizi ya dawa bandia na duni, kwa kuwa vinaaminika na wananchi wengi.

Akizungumza Julai 16, 2025, wakati akifungua kikao kazi cha wahariri wa vyombo vya habari kutoka mikoa mbalimbali, kinachofanyika katika hoteli ya JB mjini Tabora, Chacha alibainisha kuwa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari ndiyo silaha muhimu katika kuzuia bidhaa hatarishi kuingia na kusambaa sokoni.

Amesema kazi ya TMDA ni ya msingi kwa usalama wa wananchi, lakini mafanikio yake hayawezi kuwa makubwa iwapo wanahabari hawatashiriki kikamilifu kuibua, kuelimisha na kufuatilia taarifa zinazohusu ubora wa bidhaa za afya.

“Nyinyi ndio jicho na sauti ya jamii. Kupitia kalamu zenu, watu wanaelewa hatari ya dawa bandia na kujua hatua za kuchukua wanapokutana nazo,” alisema Chacha huku akiwataka waendelee kushirikiana na TMDA.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo, alisema kikao hicho kinalenga kuwajengea wahariri uelewa mpana kuhusu majukumu ya TMDA, mafanikio yaliyofikiwa na mikakati ya kukabiliana na bidhaa hatarishi.

Alisema mafanikio ya TMDA yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na ushirikiano mzuri na vyombo vya habari, na kwamba sasa huduma nyingi zimetolewa kwa njia ya kidijitali, ikiwa ni pamoja na usajili wa bidhaa na utoaji wa vibali ndani ya saa 24.

Kikao hicho cha siku mbili kinawakutanisha wahariri na waandishi kutoka mikoa ya Kanda ya Magharibi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuripoti habari za afya kwa usahihi na weledi, katika kupambana na changamoto ya bidhaa duni na bandia nchini.

spot_img

Latest articles

Yacouba atambulishwa Mbeya City

Na Mwandishi Wetu NYOTA wa zamani wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Yacouba Songne, ametambulishwa ...

Waziri Ndejembi: Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kutokana na uwepo wa vyanzo...

‘Guardians of the Peak’ kuinua utangazaji utalii wa Kilimanjaro kupitia filamu

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Guardians of the Peak, unaoingia msimu wake wa pili,...

Serikali yazindua Jukwaa la Vijana, yataja vijana kuwa mhimili Mkuu wa Maendeleo ya Taifa

Na Tatu Mohamed SERIKALI imezindua rasmi jukwaa la kitaifa la vijana lijulikanalo kama ‘Vijana...

More like this

Yacouba atambulishwa Mbeya City

Na Mwandishi Wetu NYOTA wa zamani wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Yacouba Songne, ametambulishwa ...

Waziri Ndejembi: Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kutokana na uwepo wa vyanzo...

‘Guardians of the Peak’ kuinua utangazaji utalii wa Kilimanjaro kupitia filamu

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Guardians of the Peak, unaoingia msimu wake wa pili,...