Na Mwandishi Wetu
Ofisa Habari wa klabu ya Yanga Ally Kamwe amesema licha ya kuwa yupo upande mwingine lakini ni shabiki mkubwa wa wachezaji wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala na Shomari Kapombe kutokana na uwezo mkubwa wa nyota hao.
Kamwe ametoa kauli hiyo kipindi ambacho kuna na tetesi kuwa Yanga wanaitaka saini ya Tshabalala katika kuimarisha kikosi chao.
“Nchi hii hapa hakuna mwanadamu anaweza akadharau uwezo wa Mohamed Hussein Zimbwe na Shomari Kapombe, Mimi mwenyewe ni shabiki mkubwa wa hao watu wawili ni wachezaji wazuri,” amesema Kamwe.
Hata hivyo Kamwe hajaweka wazi kuwa klabu hiyo inamhitaji mchezaji huyo baada ya kusema bado hawajaanza usajili wala kutoa orodha ya wachezaji wanaoondoka klabuni hapo.
“Kuanzia tarehe 20 mwezi huu ndiyo Yanga tutaanza kutoa taarifa rasmi ya nani katoka nani kaingia, sisi hatuna mambo ya ‘Thank You’ kipindi hiki,” amesema Kamwe.