Na Winfrida Mtoi
Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga Mtaa wa Banda Mabibo, Dar es Salaam kutokana na wingi wa mashabiki waliojitokeza kumsapoti katika maandalizi ya pambano lake la Dar Boxing Derby dhidi ya Mohammed Mpombo litakalofanyika Julai 26,2025, Viwanja Vya Leaders Club.
Tyson ambaye anatokea kambi ya Makatuni Pesa, ameweka wazi kuwa hajawahi kufeli katika mapambano yake mengi aliyocheza na kuwahakikishia ushindi mashabiki zake.
“Ukizungumzia K.O huwa inakuja yenyewe ‘automatic, sababu hata ukiangalia mapambano yangu mawili ya mwisho, la kwanza nilikuwa nacheza raundi nane lakini nikampiga mtu raundi ya pili, jingine nilicheza Morogoro katika raundi nane nikampiga mpinzani wangu katika raundi ya sita,” ametamba.

Amewaambia mashabiki zake wasisite kujitokeza siku hiyo kwa kuhofia kwani yeye amejipanga kushinda kutokana na maandalizi anayofanya.
Mmoja wa mashabiki wa bondia huyo, Hamza. Mohammed, amesema anamkubali bondia wao kwa sababu siku zote hawana kazi mbovu na ameshuhudia hilo mazoezini na ulingo utasema siku hiyo.