TPDC yapata Tuzo ya Taasisi Bora Sabasaba kwa miaka mitano mfululizo

Na Tatu Mohamed

SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeandika historia kwa kutwaa tuzo ya Taasisi Bora za Umma katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ikiwa ni mara ya tano mfululizo kushinda tuzo hiyo kutokana na ubora wa huduma na uwajibikaji wake kwa wananchi.

Tuzo hiyo imetolewa kama uthibitisho wa mchango wa TPDC katika kuimarisha uwazi, ubunifu na utoaji wa huduma bora ndani ya sekta ya nishati nchini.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya ufunguzi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TPDC, Maria Mselemu, alisema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya utendaji kazi bora, nidhamu ya kiutendaji na ufuatiliaji wa karibu wa miradi inayosimamiwa na shirika hilo.

“Hii ni tuzo yetu ya tano mfululizo katika maonesho ya Sabasaba. Ubora wa huduma zetu, miradi ya kimkakati na mchango wetu katika utunzaji wa mazingira umekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio haya,” alisema Mselemu.

Aliongeza kuwa TPDC imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza utoaji wa hewa ukaa kwa kuhimiza matumizi ya nishati safi, hususan kwa matumizi ya majumbani na kwenye magari.

“Tayari tumeondoa zaidi ya tani 100,000 za hewa ukaa kupitia juhudi zetu za kusambaza gesi asilia. Ni mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi,” alieleza.

TPDC pia imewahi kutwaa tuzo ya mazingira kutokana na juhudi zake katika kulinda na kuhifadhi mazingira kupitia matumizi ya nishati mbadala, jambo linaloendelea kuipa heshima shirika hilo miongoni mwa taasisi za umma.

Maonesho ya Sabasaba yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kuonesha ubunifu, huduma na bidhaa bora kwa Watanzania, huku yakitoa fursa kwa mashirika kama TPDC kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...