Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Gf Trucks & Equipment imeibuka mshindi wa jumla katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba 2025 , kupitia kiwanda chake cha kuunganisha magari makubwa cha GF Vehicle Assemblers(GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani
Katika maonesho hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam, yameshirikisha makampuni na wafanyabiashara mbambali wa ndani ya chini na nje kama vile China, Korea, Uturuki , Ulaya na Afrika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussen Ali Mwinyi alizindua maonesho hayo jana Julai 7,2025 ambapo alitembelea baadhi ya mabanda kabla ya kuanza kutoa tuzo na zawadi kwa washindi.

Miongonj mwa mabanda aliyotembelea ni Rais Mwinyi nj la GF na kujionea bidhaaa mbalimbali zinazouzwa na kampuni hiyo ambazo magari madogo ya Hyundai, Mahindra, magari makubwa aina ya FAW , mashine na mitambo ya XCMG.
Pia alijionea jinsi michakato ya awali ya uunganishaji wa magari unavyofanyika kupitia kiwanda cha kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa kutoa tuzo hiyo, Rais Mwinyi aliwapongeza GF kwa kuibuka kuwa vinara wa maonyesho hayo na kuwataka wasibweteke na kupanua zaidi katika uwekezaji, huku akiwakaribisha Zanzibar.

Naye Mkurugezi wa kampuni ya GF ,Ali Karmali amesema wanajivuni kuwekeza nchini kama kiwanda cha kwanza cha kutengeneza magari ya aina zote kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na Serikali kwa wawekezaji.
“Tunajivunia kuwa waongoza njia na makampuni mengine yajifunze kwetu kupitia kiwanda chetu cha kuunganisha magari na tupo katika awamu ya tatu ya upanuzi itakayochukua zaidi ya wafanyakazi 3000 hivo kuongeza ajira kwa watanzania,” amesema.


