Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Kusimamia Ubora wa Mikataba ya Umma kwa Maslahi ya Taifa

Na Tatu Mohamed

OFISI ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kutoa ushauri wa kisheria kwa taasisi za umma ili kuhakikisha mikataba inayosainiwa na serikali inakuwa na ubora, inatekelezwa ipasavyo na inazinufaisha jamii.

Kauli hiyo imetolewa Julai 07, 2025 na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Samwel Maneno alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.

“Tunaendelea kuzipa ushauri taasisi za umma ili kuwa na mikataba yenye ubora na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa mujibu wa makubaliano,” alisema Maneno.

Ameongeza kuwa maonesho ya Sabasaba ni jukwaa muhimu kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa huduma kama ushauri wa kisheria, kushughulikia malalamiko ya wananchi, pamoja na elimu kuhusu sheria zilizofanyiwa marekebisho, toleo la mwaka 2023, ambazo zimeanza kutumika rasmi kuanzia Julai 1, 2025.

“Katika sheria 446 zilizofanyiwa urekebishaji, zaidi ya sheria 300 tayari zinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, jambo ambalo linaongeza uelewa wa wananchi kuhusu sheria,” alifafanua.

Katika ziara yake, Naibu Mwanasheria Mkuu pia alitembelea mabanda ya Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria na Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, kujionea namna taasisi hizo zinavyoshiriki katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Maonesho ya Sabasaba 2025 yamezinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, na yanatarajiwa kumalizika Julai 13, 2025.

spot_img

Latest articles

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...

Chipukizi wa kuogelea kushindana ‘ East Africa Development Swimming Gala’

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya waogeleji 600 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya chipukizi...

More like this

Muswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Umma kukamilika 2026/27

Na Mwandishi wetu KATIKA kuendelea kuimarisha uwekezaji wa umma, Serikali imepanga kukamilisha Muswada wa...

Kocha Bilo afariki dunia

Na Mwandishi Wetu MMILIKI wa Kituo cha Soka cha Bilo Jijini Mwanza, Kocha Athuman Bilal...

Tukatae kunyweshwa sumu hii

“Kama taifa letu lilipata kuwa na bahati ni kuwa na Rais aliyechukia rushwa kama...